top of page

St. Cecilia Mass- Dandora



BWANA UTUHURUMIE.

v Bwana Bwana – Ee Bwana tuhurumie (Ee Bwana) tuhurumie (Bwana) – (na) tuhurumie Ee Bwana tuhurumie.

v Ee Kristu (stu) tuhurumie (x3)… x2

v Bwana

v Ewe – Bwana Ee Bwana tuhurumie x4


UTUKUFU.

  1. Utukufu juu kwa Mungu utukufu juu mbinguni – na amani duniani kwa wenye mapenzi.

Tunakusifu Baba (wewe) twakuheshimu twakuabudu Baba (sisi) twakutukuza x2

  1. Wewe ni Mungu Baba Mfalme Baba Mwenyezi Kristu wa Yesu Bwana Mwana pekee Mungu.

  2. Ewe ni Yesu Kristu Mwana Kondoo wa Mungu mwenye kuziondoa dhambi ‘tuhurumie.

  3. Mwenye kuziondoa dhambi za watu wote mwenye rehema nyingi ombi letu pokea.

  4. Mwenye kuketi kwake kuume kwa Mungu Baba tupe huruma zako wewe Mtakatifu.

  5. Ewe ndiwe Bwana we mkuu we Bwana wetu Mkombozi Yesu Kristu wewe peke yako.

  6. Pamoja naye Roho Mtakatifu we Bwana katika utukufu Mungu milele yote.


NASADIKI.

  1. BASS:- Nasadiki kwa Mungu moja – Ninasadiki

ALL:- Ndiye Baba yetu Mwenyezi – Nasadiki Ninasadiki.

BASS:- Nasasiki kwa Mungu muumba – Nina…

ALL:- Muumba mbingu pia dunia – Nasa…

Nasadiki – ninasadiki (mimi) nasadiki kweli ninasadiki.

  1. Nasadiki kwa Bwana Yesu Kristu / ndiye Mwana pekee wa Mungu / - mwenye kuzaliwa kwa Baba, akapata mwili kwa tendo / lake Roho Mtakatifu – kazaliwa naye Bikira.

  2. Kisha yeye kusulubiwa / kwa amri ya Ponsyo Pilato – akateswa akafa / - akazikwa na kuzimu akashukia / kafufuka siku ya tatu – akapaa kule mbinguni.

  3. Ameketi kuume kwa Baba / ndipo atakapotokea – kuhukumu wazima na wafu, kwake Roho Mtakatifu / na kanisa la katoliki – takatifu la hao mitume.

  4. Ondoleo la dhambi zetu / nangojea ufufuko wa mwili – na uzima wake milele.


BABA YETU.

Baba yeu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. Falme (ee) wako (ee) Baba ufike, utakalo lifanyike.

1. Mapenzi yako na yatimizwe – utakalo lifanyike duniani kama mbinguni – utakalo…

2. Utupe leo mkate wetu… Mkate wetu wa kila siku…

3. T/B:- Utusamehe makosa yetu…

S/A:- Nasi tuwasamehe wenzetu walio tukosea sisi…

4. Usitutie kishawishini…utuokoe kwenye maovu…

5. Kwani ufalme ni wako Baba… Nguvu ‘tukufu hata milele…


MTAKATIFU.

Mtakatifu x2 – (Mtakatifu x3) Bwana Mungu wa majeshi hata mbingu na dunia – hata mbingu na dunia zimejaa utukufu

wako ee Hosana juu mbinguni.

Hosanna – (Ee Hosanna x2) juu mbinguni x2.

Mbarikiwa ‘naye kuja kwa jina lake Bwana x2.


MWANA KONDOO.

Ee Mwana Kondoo – Ee Mwana Kondoo x2 wa Mungu. Ewe – uondoaye dhambi za dunia utuhurumie . Ewe Bwana. Ee Mwana Kondoo – (Ee Mwana Kondoo x2 wa Mungu… Ee utujalie amani x2 (wewe x2) (Ewe){U} tujalie amani x2

39 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page