top of page

Simameni Tupeleke


Simameni waumini wote tupeleke vipaji vyetu vyote kwake Muumba kwani mali yake x2 Baba (tumebeba mali yetu tunaleta kwa furaha twakuomba Mungu mwenye enzi uipokee, ni mapato ya kifedha ni mazao ya mashamba tunaleta kwako

  1. Sadaka ni mapato Baba uliyotujalia, nasi tunaileta kwako kama shukrani yetu, twakuomba Mwenyezi uipokee leo, mikononi mwa padre sadaka yetu hii, kisha utubariki kwa Baraka ya-ko, na ile yake mwana, na ya Roho Mtakatifu.

  2. Maisha mazuri Baba sisi tunajivunia, afya njema ya mwili na roho pia umetupa, basi tunajileta kwako kama dhabihu, hivyo ikupendeze kwani ni mali yako, Ba-ba twakuomba utupokee- leo, na kisha utubariki tuende tumetakasika.

  3. Tunapoleta mapato haya Baba twatimiza, wajibu wetu kwako na pia kwa kanisa letu, Baba twafurahia mapendo yako kwetu, pia tunashukuru kwa Baraka za-ko, na sasa twakuomba uwatembe-lee, wasiojiweza nao ukawabariki.

  4. Tunawaombea wale wenye mioyo migumu, wasiopenda kutoa zako ya mapato yao, uwatumie Roho yule msaidizi, ili awakumbushe majukumu ya-o, yakuleta chakula kwa nyumba ya-ko, na kujenga kanisa kanisa lako wewe.

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page