top of page

Siku ya Ubatizo Wangu

  1. Siku ya ubatizo wangu, nilimuahidi Mungu, nitamfuata Yesu Kristu, ndiye uzima kweli dini ya kweli neema kuu nitaishika hio tu, milele siikani

  2. Mbali shetani akimbie, si mtumwa wake tena, nadhiri yangu niishike, nitashindana vyema, adui mbaya namkataa, furaha zake na tamaa, milele simfuati

  3. Yesu Mkombozi yumo hapa, kwa mwili na kwa damu, Ye mwana wa mwenyezi Baba na pia mwanadamu, naiamini sii kuu, sababu ya Imani tu, milele nisadiki

  4. Yesu mchungaji anijia, miye maskini dhaifu, nguvu apate kunifia, kwa mkate mtakatifu, namtumaini yeye tu, nampenda kwa shukrani kuu, milele nitamsifu

66 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page