top of page

Siku Nzuri Kuna Nini


Siku nzuri kuna nini duniani watu wote Duniani watu wote leo shangwe Mnieleze leo shangwe ya nini Mnieleze leo shangwe ya nini


Siku nzuri kuna nini na kelele za vifijo Na kelele za vifijo zasikika Mnieleze leo shangwe ya nini Mnieleze leo shangwe ya nini


Ni furaha tele, na sherehe kubwa Ulimwengu, umefanya sherehe kubwa Mbinguni malaika wanaimba nyimbo nzuri Tamu za kupendeza, twende tukaona


Kuna nini pangoni Bethlehemu, Kazaliwa mtoto mzuri mpole na mnyenyekevu Twende tumsalimu


Huyu mtoto ndiye Mwana wa Mungu Huyu mtoto ndiye Yesu Kristu


Ni Yesu Kristu, amekuja kwetu, amekuja kutukomboa sisi Kweli ni furaha kubwa mno


Ni Yesu Kristu, amekuja kwetu, amekuja kutukomboa sisi Kweli ni furaha kubwa mno

Tuimbe aleluya leo, tuimbe aleluya leo Tuimbe aleluya leo, tuimbe kazaliwa Bwana Aleluya tuimbe kazaliwa Bwana


Ulimwengu, umefanya sherehe kubwa Mbinguni malaika wanaimba nyimbo nzuri Tamu za kupendeza, twende tukaona


Kuna nini pangoni Bethelehemu, Kazaliwa mtoto mzuri mpole na mnyenyekevu twende tumsalimu

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page