top of page

Sifa Sufuufu


1. Maria mama wa mungu tena mama yetu Sisi Wana wa dunia tunakuja kwako twakuja na nyimbo zetu nazo Ngoma zetu twakuchezea twakuimbia Kwa shangwe


((Twakumiminia (Sifa) ×2 sufufu Maria ) ×2

Mwanao twakupa (sifa) ×2 sufufu Maria

Twakumiminia ( sifa) ×2 sufufu uzipokee ) ×2) ×2


2. Pokea salamu zetu ewe mama mwema umejawa na neema Bwana Yuko nawe umebarikiwa wewe kuliko wengine wewe ni mama wamwokozi wa dunia


3. Bikira usie na dhambi mama msafi chemichemi ya faraja malkia wa mbingu malkia wa rozari na nyota ya bahari nyota ya asubuhi kimbilio letu


4. Mama mwenye huruma nyingi mama mpole wewe ni mwenye huruma na mpendelevu utuongoze Sisi tulio safarini hadi tufike mbinguni uliko wewe

12 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page