top of page

Shetani Katimua Mbio

1. Hapo ndipo tulipomfurahia Bwana Mungu wetu; Hirizi na mizimu yote viliposhindwa kusimama, shetani naye kivumbi kakitimua kakimbia.

Hapo ndipo tukasema Mungu aitwe Mungu.

Hapo ndipo tukasema Mungu apewe sifa.

Hapo ndipo tukasema atawale Mungu milele x2

2. Tazama Bwana alipounyosha mkono wake mkuu, wachawi wote wakakoma mapepo na yakanyamaza, waganga na tunguli zao kwa aibu wakaduwaa.

3. Bwana alipoinua mkono wake hodari kwa wagonjwa, wakoma wote wakapona viziwi na wakasikia, viwete wakarukaruka kwa furaha wamepona.

4. Jicho la Bwana lilipowaelekea watu waovu hasira, chuki na majivuno vyote vikatoweka, kiburi na maringo yao hapo ndipo vikapotea.

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page