top of page

Shangwe Kwake Mfufuka


Ni furaha Yesu kafufuka mkombozi wetu kashinda mauti x2 Utukufu sifa na heshima (kweli)ni kwake yeye kashinda mauti x2

  1. Kweli Bwana Yesu amefufuka mzima, kwani kaburini hayumo tena, amefufuka alivyosema natufanye sote ni shangwe

  2. Naye malaika akawatokea, wale kina mama pale kaburini, kawauliza mbona mwamtafuta, al'e hai kati ya wafu

  3. Akawatokeya watumishi wake, wakiwa bado wamejazwa na hofu, akawaambiya amani iwe kwenu, kawajaza Roho Mtakatifu

  4. Kumbukeni Yesu alivyosema,l ivunjeni hili hekalu lake Mungu, nami nitalijenga kwa siku tatu, kwa hakika kayatimiza

11 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page