top of page

Sekwensia

  1. Uje Roho mtakatifu, tuangaze toka Mbingu, roho zetu kwa mwangao

  2. Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji, uje mwanga wa mioyo.

  3. Ee mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana, ewe raha mstarehe.

  4. Kwenye kazi upumziko, kwenye joto burudisho, u mfutaji wa machozi

  5. Ewe wanga wenye heri, uwajaze waamini, neema yako moyoni

  6. Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu, kwake yote yana kosa

  7. Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu, na kuponya majeraha

  8. Ulegeze ukaidi, pasha moto ubaridi, nyosha upotovu wote

  9. Wape waamini wako, wenye tumaini kwako, paji zako zote saba

  10. Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila ila, wape heri ya milele

  11. Amina aleluya, amina aleluya, amina aleluya

5 views0 comments

Bình luận

Đã xếp hạng 0/5 sao.
Chưa có xếp hạng

Thêm điểm xếp hạng
bottom of page