top of page

Sasa Wakati Umefika




Sasa wakati umefika wakushika nilichonacho (mimi) kwa wema niende kwa Mungu nitoe zawadi , Sasa wakati umefika kwenda mbele ya Mungu wangu (mimi) aone nilivyo anadaa zawadi ya leo. Nitamwambia Bwana pokea (hiki) kidogo nilicho nacho Kwani Mungu wewe wanijua (mimi) siwezi hata kueleza Nakusihi sana Baba unipokee, Nigawie Baraka niwe salama


1. Mema yote nilivyo kuwa nayo yametoka kwaMungu, hivyo nami nikosa kusahau kumshukuru, Kwani kuwe po hapa leo hii ni kazi nani? Kamwe mimi sitapata uwezo pasipo Mungu.


2. Mema aliyotenda Mungu nijibu lini na vipi? Mbona hofu ya zidi kuwa ndani ya moyo wangu, Mbele za Bwana Mungu kufanya siri ni bure, Yeye ndiye mpanga mambo yote ya wanadamu


3. Pumzi inayonipa uhai inatoka kwa nani? Bila Mungu hakika mwanadamu siwezi kitu, Nimepata nafasi leo ya kwenda kutoa zawadi, Heri niende ya kesho siyo yangu ajua Baba


4. Ewe muumba wa vyote duniani na vyote vya mbinguni, Mimi leo nakuja kwako Baba nihurumie, Baba we ndiwe unayetawala kulala na kuamka kwangu, juu yangu utake nini Baba kisifanyike!





35 views0 comments

Commenti

Valutazione 0 stelle su 5.
Non ci sono ancora valutazioni

Aggiungi una valutazione
bottom of page