top of page

Salamu Maria

Salamu Maria, salamu mbarikiwa, Bikira daima, na Mama yake Yesu Kristu Ewe Mama utuombee, kwa mwana wako Yesu Kristu, sisi wanyofu wamoyo, twakusihi sana x2

1. Ulitafuta , Yesu kwa huzuni kuu, alipokwenda, hekaluni kamkosa,

Unitafute, dhambi zinaponificha, unirejeshe, kwa pendo lake Bwana.

2. Ulitembea, nyumbani kwa Elzabeti, moyoni mwake, kakutana na Yesu,

Ni tembelee, ili pia moyo wangu ushuhudie, upendo wake Kristu.

3. Ulimfuata, Bwana Yesu kalvari, alipobeba, msalaba wa dhambi,

Unifuate katika mateso yangu, ili niweze, kumshinda shetani

4. Ulimtazama, mwanao msalabani juu, kwa huzuni kuu, bali pasipo shaka,

Usiniache, mauti yakinisonga, na unilaki, siku ya kufa kwangu.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page