top of page

Pokea Sifa Zangu


Ninakupenda Mungu (wangu) ninakupenda wewe milele na milele (Bwana) nitakutukuza Pokea sifa zangu (Bwana) zinazotoka katika kinywa changu mimi (ndani) na moyoni wangu x2

  1. Katika makusanyiko nitaziimba zaburi Nitazitangaza sifa zako daima milele Kwenye madhabahu yako nitaitoa sadaka Ile ya kukupendeza ee Mungu Muumba wangu.

  2. Umenitendea mengi, mema yasiyo idadi Ninakushukuru Bwana, ee Baba Muumba wangu Nikiyakumbuka yote, machozi yanimwagika Ni machozi ya furaha, ni machozi ya upendo.

  3. Usiniache ee Bwana, na wala usinitupe Ukinitupa wewe, nani ataniokota Ndiwe msitiri wangu, katika dunia hii Dunia yenye mateso na yenye mahangaiko

12 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page