top of page

Pilika Pilika


  1. Pilka pilka kila siku watu wa dunia Wanahangaika kutafuta mali za dunia Asubuhi ni msongamano, mchana vilevile Usiku shughuli zafanyika kama kawaida Tafuteni kwanza ufalme ule wa mbinguni Na hayo mengine (hakika) mtazidishiwa (Yeye Mungu (Mwenyezi) mtetezi (ajabu) Mkiamini atawashughilikia) x2

  2. Pilika pilika watu wengi kutafuta elimu Hawakumbuki kwamba Yesu ni mwalimu tosha Ajali nyingi barabarani zinafanyika kwetu Tumesahau kwamba Yesu ni dereva tosha

  3. Pilika pilika twatafuta hospitali kubwa Huku daktari mkuu ni Mungu wa majeshi Watu watafuta waganga ili wapate mali Bali Mungu wa mbinguni ndiye mmliki wa vyote

  4. Pilika pilika tunawaza usiku na mchana Vile tutakula vizuri na kuvaa vizuri Kwani ndege wale wa angani wanalishwa na nani Kama siyo Mungu wa mbinguni basi huyo nani

  5. Pilika pilika wenzangu tumuelekee Mungu Tusifadhaike bali tuwe na matumaini Atatujalia mema mengi tukiwa duniani Mwisho tutafurahi na Yesu kule juu mbinguni

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page