top of page


Ni mazao ya mashamba nazo fedha za mifuko ni mkate na divai tunaleta kwako Baba x2

  1. Nikikumbuka pendo lako ee Yesu wangu (kweli) machozi ya furaha yananitoka. Jinsi ulivyonifilia msalabani (kweli) nafsi yangu ipate kukombolewa.

  2. Pendo la Bwana Yesu ni pendo la ajabu (kweli) ni pendo la agape pendo la Mungu. Kajitolea kwetu bila hata malipo (Bwana) kafa msalabani kwa ajili yetu.

  3. Tazama jinsi ilivyo vyema na tena vizuri (sana) ndugu kuishi pamoja kwa amani. Tuwapende wenzetu kama tunavyojipenda (sisi) vile Mungu mwenyewe anatupenda.

  4. Tumesikia torati ya kale inavyosema (kwamba) mpende jirani yako akupendaye. Walakini umchukie adui yako kweli (kweli). Kwani ni jicho kwa jicho jino kwa jino.

  5. Tumepewa amri kuu ya upendo wa Mungu (Baba) tuwapende wenzetu kwa moyo wote. Tuwapendeni adui zetu na kuwaombea (sana) waishi kuziona Baraka za Mungu.

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page