top of page

Pangoni pangoni siyo tena kwenye wanyama watupu kwenye wanyama tu huko kuna Mungu huko pamoja na sisi x2

Pangoni kuliko duni ndiko yuko Mungu tukampokee

Pachafu ndiko yuko Mungu tukampokee

Tena gizani ndiko yuko Mungu tukampokee

Baridi kali ndiko yuko Mungu tukampokee


  1. Mama yake Binti mwali Bikira wa familia duni ni mlinzi wake ni seremala fundi wa kawaida hivi mashuhuda ni wachungaji harufu ni ya samadi ulaula huyo ndiye Yesu huyo ndiye Mungu pamoja nasi

  2. Daima wapendwa tuache makuu twende kule kuliko duni sana kwa washamba wajinga na fukara twendeni wote Huko ndiko kunakozaliwa Mungu huko ndiko anako waijia watu huko ndiko pangoni pa kila siku huko ndiko anakozaliwa Yesu

  3. Na tukisha fika kule kwenye pango tumtolee zawadi zenye upendo tuimbe tuimbe tuimbe nyimbo nzuri kwa shangwe kuu tucheze tucheze tucheze ngoma za furaha

Anastahili vigelegele na makofi tena anastahili vigelegele na makofi yeye ndiye anastahili vigelegele na makofi


67 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page