top of page

Onjeni Muone



Onjeni muone Bwana - Onjeni muone yu mwema x2 Onjeni Mungu Baba (kweli) Onjeni muone yu mwema Onjeni Yesu Kristu (kweli) Onjeni muone yu mwema x2

  1. Jiungeni enyi viumbe Mbinguni na duniani Tuliadhimishe jina lake Mungu Baba kwa pamoja Kwa kinanda na filimbi, kwa sauti ya baragumu Kwa vinubi na zeze na ngoma na nyimbo

  2. Mtukuzeni Bwana Mungu kweli pamoja nami Tumshangilie kwa furaha katika hekalu lake Tafuteni Bwana Mungu naye Bwana atawajibu Atawaponya wote na dhaabu zenu

  3. Nitamhimidi Bwana Mungu wangu siku zote Sifa zake zote zi kinywani mwangu daima Kwa Bwana Mungu wangu, nafsi yangu itajisifu Wenye haki wasikie wakafurahi

  4. Elekezeni macho juu, nanyi mtatiwa nuru Wala nyuso zenu siku zote kamwe zisione haya Onjeni Mungu Baba onjeni na Yesu Kristu Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema

9 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page