top of page

Nyumbani Mwa Mungu

(Nyumbani mwa Mungu mwema mwakaribishwa, Baba wa watu wote tukamwabudu)x2

Twende sote ni mwaliko wa kila taifa Twende sote ni mwaliko wa kila kabila


1. Neema fadhili huruma…. Ah

Ni nyingi kwa wote wamchao…. Ah

Twendeni mbele zake kwa mioyo wazi, Na yeye atatupa mapendo rohoni.


2. Tungie kwa nyimbo za shukrani…Ah

Tujongee kwa nyimbo za sifa…….Ah

Matendo yako Mungu ni mengi sana, Dunia na vijaavyo ni uwezo wake mkuu.


3. Yeye ni Mungu wa Abrahamu….Ah

Yakobo, Melkizedeki na Musa….Ah

Kajaa toka juu na pia chini, Kwa imani tumwabudu na tukamsujudu.


4.Twendeni mlio na njaa….. Ah

Twendeni mlio na kiu…… Ah

Twendeni kwa karamu ya Mwanakondoo, Malipo ni bure ni Yesu Mwokozi.


5.Tumsifu Mungu Baba mwema…. Ah

Tumsifu Mungu Mwana wake….Ah

Na Roho Mtakatifu mleta uzima,Kama mwanzo sasa na siku zote daima

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page