top of page

Nyumba ya Roho

Mungu wangu nikujue mimi, Mungu wangu nikupende Mungu nikutumikie, kisha niurithi ufalme Mbinguni x2 (wewe) roho umenipa ee, (kisha) ukaihifadhi vizuri (yaani) ndani ya mwili ee (kwani) mwili ni nyumba ya roho

  1. Ndiwe mungu peke yako, wa kuabudiwa ni wewe nishike kitakatifu siku hiyo siku yako nisilitaje kabisa bure jina lako Mwenyezi Ulimi wa mwili wangu usiiponze roho yangu

  2. Niwaheshimu wazazi, ili nisiwasononeshe uhai wa binadamu niuthamini yani nisiuue kuiba nijiepushe, kusema uwongo niache Mwili wangu usizini ndipo roho yangu itapona

  3. Niepuke kutamani yote yasiyo mali yangu naye mwanamke asiye mke wangu yani sio wangu Hapo ndipo nitakuwa nimeutumia vizuri mwili ulioiumbia roho ifike Mbinguni juu

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page