top of page

Nyote Mmekaribishwa

Nyote mmekaribishwa. Nyumba yake Bwana Mungu kwa furaha tuingie.

Tumwabudu Mungu wetu Kwa nderemo na makofi shangwe na vigelegele,

TumwabuduBwana tumwimbie kwa nderemo na makofi shangwe na vigelegele x2

1. Akina mama shangilieni kwa sauti kuu, nyimbo zenu zisikike ulimwenguni.

2. Nanyi waume msichoke kurukaruka, furaha yenu isambae dunia kote.

3. Watoto wote inukeni mbele za Bwana, mkionyesha tabasamu usoni mwenu.

4. Vinanda ngoma na kayamba vipigwe sana, Mungu wetu afurahi juu mbinguni.

5. Walei watawa na mapadre msiwe nyuma, ongozeni watu wote twende mbinguni.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page