top of page

Nyota ya Mashariki



  1. Kakukirimia, uwe ulivyo, Atakutumia impendezavyo Akikuinua, inuka, hivyo, Ninakuombea heri vilivyo; Hakunipa hayo, nikuhitaji, Kwa niliyo nayo, upate maji, Na mwisho wa hayo, tuvikwe taji, Tuingie nayo, wa mbingu mji.

  2. Sirudi kwa njia, yake herode, Anakuvizia, kila upande, Wivu unamjia, kakunja, konde, la kukuzuia juu usipande; Ni kama Kaini, mwua Abeli, au Raubeni, wa Israeli, Waliotamani, kuzika, hali, Ya wadogo duni, wake Jalali!

  3. Ninakuombea, usife moyo, Maana dunia, si rafikiyo, Wewe fuatia, za Kristu, nyayo, Aliyekufia, kwa mizigoyo; Wa ulimwenguni, watakufumba,Wazuri machoni, moyo mwembamba, Hawatatamani, uitwe, mwamba,Ni wivu moyoni, unawasomba!

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page