top of page

Nyota ya Bahari



  1. Bara na bahari furahini sana Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni Bara na bahari furahini sana Tumemulikwa na nuru ya Mbinguni

  2. Pendo lako mama, limetuvutia, Tunatangaza sifa zako kwa nyimbo Bara shangilia, bahari ivume, Tumsifu mama, mama wa Maulana

  3. Piga tarumbeta, pigeni mluzi, Imbeni wimbo wa mama wa Mulungu chezeni pamoja, ruka juu juu, Mama wa Yesu afurahi Mbinguni

  4. Mama wa Mwokozi, Malkia wa Mbingu Mwanga anamu somo wa kwaya yetu uliyekingiwa dhambi ya asili, Daraja letu tuendao Mbinguni

  5. Nyota za angani zamulika nchi, Mama Maria anamulika nyoyo usiku mchana anatuangaza, Tunatembea na nuru siku zote

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page