top of page

Njooni Tuingie

Njooni wote tuingie nyumbani mwa Bwana, njoni wote tumwabudu na tumsifu Mungu x2

  1. Twende watu wote twendeni nyumbani mwa Bwana (Mungu) tujongee na sala pia na sadaka zetu (Kweli) tutapata nazo Baraka na neema tele (Tele)

  2. Twende kina baba twendeni nyumbani mwa Bwana (Leo) twendeni na ngoma kayamba pia tarumbeta (zetu) tumusifu Mungu muumba wa mbingu na nchi (yote)

  3. Twende kina mama twendeni nyumbani mwa Bwana (twende) tumuinue Mungu maana tumwimbie Mungu maana ni mweza wa yote (Kweli) tukatoe shukrani zetu kwake Mungu Baba (yetu)

  4. Twende na vijana twendeni nyumbani mwa Bwana (Tena) kwa sauti zetu na tamu zimpambe yeye (Mungu) tuungane na malaika wa kule mbinguni (juu)

18 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page