top of page

Njoni Wapenzi

Njoni wapenzi tufanye shangweMwokozi Bwana amezaliwa

Viumbe vyote tufanye shangwe Mwokozi Bwana amezaliwa


Natufanye shangwe, twimbe aleluya, Mwokozi Bwana amezaliwa


Malaika alitutangazia Mwokozi Bwana amezaliwa

Furaha yetu ni kubwa sana Mwokozi Bwana amezaliwa


Twende pamoja na wachunga Mwokozi Bwana amezaliwa

Tumwone mtoto Yesu pangoni Mwokozi Bwana amezaliwa


Yeye ni kweli Mwana wa Mungu Mwokozi Bwana amezaliwa

Mapendo yake hayana mwisho Mwokozi Bwana amezaliwa


Hii ni siku ya furaha kuu Mwokozi Bwana amezaliwa

Mungu mwenyewe atushukia Mwokozi Bwana amezaliwa


Tufanye shangwe kwa nyimbo nzuri Mwokozi Bwana amezaliwa

Tumsifu Bwana na kumshukuru Mwokozi Bwana amezaliwa


Sisi kwa sisi na tupendane Mwokozi Bwana amezaliwa

Tulifuate pendo la Yesu Mwokozi Bwana amezaliwa

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page