top of page

Njoni Tumwimbie

Njooni tumwimbie Bwana wetu - kwa shangwe njooni kwa masifu kwa nderemo - tucheze (Njooni tuabudu, njooni tusujudu, tupige makofi, Mbele zake Bwana, Mungu wa ulimwengu) x2

  1. Hekalu lake Bwana Mungu linapendeza, Nyumbani mwake Bwana mna mengi mazuri Ninatamani kuingia nyumbani mwake Nikae naye siku zote nyuani mwake Nipate heri, mbele za Bwana

  2. Mapema leo ninabisha lango ee Bwana Nifungulie nipokee nipe faraja Nimelemewa na mizigo mingi ya dhambi Nyumbani mwake Bwana ndiko kuna uzima Uzima tele, na usalama

  3. Twendeni sote kwake Bwana Mungu Mwenyezi Twendeni kwake tupeleke maombi yetu Tutoe shukrani zetu kwa Mungu BabaTutoe na dhabihu zetu kwake Muumba Sadaka zetu, azipokee

  4. Uhai wetu unatoka kwake Muumba, Tuimbe sifa zake Mungu siku kwa sikuTuyatangaze maajabu yake popote Tuseme Bwana ametenda mambo makuu Kwa watu wote, milele yote.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page