top of page

Njiani Huniongoza

Njiani huniongoza Yesu wangu, Mwokozi:

Rehema hatapunguza, Milele Kiongozi.

Ina raha kwandamana Duniani daima:

Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema.


Njiani huniongoza Hupunguza matata;

Nikiungua hupoza. Na njaani nashiba.

Lichokapo guu langu Nguvu zikapungua.

Jiwe lilo mbele yangu hunibubujika.


Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,

Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu,

Nikivikwa kutokufa, Nikae na Mwokozi,

Nitamsifu sana; sifa: ‘ Kweli ni Kiongozi.‘

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page