top of page

Njia ya Msalaba

Tufwate njia ya msalaba,

tuifwate mpaka kalvario,

tusimamepo bila haya.

(msalaba) msalaba uponya roho x2


1. Umekosa nini we Yesu,

Kushtakiwa bure kwa Pilato,

Wenye kustahili hukumu

(si wewe) si wewe Bwana ni sisi x2


2. Ole msalaba huo mzito,

Apagazwa mwana mpenzi wa Mungu,

Mwili waenea mateso,

(alipa) alipa madhambi yetu x2


3. Ona muumba wa mbingu na nchi,

Yupo chini mzigo wamlemea,

Na mtu kiumbe chake kwa ukali,

(ampiga) ampiga bila huruma x2 .


4. Huko njiani we maria,

Waonaje hali ya mwanao,

Ni damu tupu na vidoda,

(machozi) machozi yamfumba macho x2.


5. Kwa Simoni heri ya kweli,

Mimi pia Yesu nisaidie,

Kuchukua mzigo wa ukombozi,

(kuteswa) kuteswa pamoja nawe x2.


6. Uso wa Yesu malaika,

Betlehemu walikuabudu,

Bahati yake Veronika,

(kupaguza) kupaguza mfalme wa mbingu x2.


7. Wakimvuta huku na huku,

Wauaji wanamchokesha bure,

Chini wamtupa bado kwa nguvu,

(aibu) aibu yao milele x2.


8. Wanawake wa Israeli,

Msilie kwa sababu hio,

Muwalilie hao kwa dhambi,

(upanga) upanga ni juu yao x2.


9. Mwokozi sasa ni ya tatu,

Waanguka chini ya msalaba,

Katika dhambi za uregevu,

(nijue ) nijue kutubu hima x2


10. Muje malaika wa mbingu ,

Funikeni mwiliwe kwa huruma,

Vidonda vyake na utupu

(askari) askari wamemvua x2


11. Hapo mkristu ushike moyo,

Bwana wako alazwa msalabani,

mara miguu na mikono,

(yafungwa) yafungwa kwa misumari x2.


12. Yesu nakuabudu ,

Msalabani unapohangaika,

Nchi yatetemeka kwa hofu,

(na jua)na jua linafifia x2.


13. Mama maria mtakatifu,

Upokee maiti ya mwanao,

Tumemwua kwa dhambi zetu,

( twa-tubu ) twa-tubu kwake na kwako x2.


14. Pamoja nawe kaburini,

Zika dhambi na ubaya wa moyo,

Yesu tuwe wakristu wa ukwweli,

(twakupa) twakupa sasa mapendo x2.


15. Katika Roho yangu Bwana,

Chora mateso niliyokutesa,

Nisiyasahau madeni,

(na kazi) na kazi ya kuokoka x2

2 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page