top of page

Nitamwimbia Bwana

Nitamwimbia Bwana (Bwana wangu) Nitamwimbia Bwana kwa kuwa ametukuka sana!


Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu

(nasema) Bwana ndilo jina lake.

Amekuwa wokovu wangu hakika,

(nasema ) Bwana ndilo jina lake.


Mpanda farasi naye farasi wake

Bwana amewatupa kwenye bahari

Yeye ni Mungu wangu nitamsifu

Mungu wa baba yangu nitamtukuza


Gari lake faraho na jeshi lake

Bwana amewatupa kwenye bahari

Maakadi yake wateule wote

Wamezama katika bahari ya Sham


Mkono wa kuume wa Mungu Mwenyezi

Umepata fahari ya uwezo

Mkono wa kuume wa Mungu Mwenyezi

Umewasetaseta adui zake


Kwenye mlima ambao amechagua

Atamwingiza Sioni na kumpanda

Pale alipojenga kwa mkono wake

Naye atutawale sisi milele

3 views0 comments

Kommentare

Mit 0 von 5 Sternen bewertet.
Noch keine Ratings

Rating hinzufügen
bottom of page