top of page

Nitalisifu Jina


Nitalisifu Jina lake Mungu kwa wimbo wangu, nami nitamshukuru yeye siku zote, kwa sababu Bwana ananipenda daima, amenipa uzima na amenibariki x2


  1. Watu wote njooni leo Tuimbe kwa shangwe, mbingu na dunia njoni Tuimbe kwa shangwe, njoni mbele zake Bwana Tuimbe kwa shangwe

  2. Tangazeni sifa zake Bwana anatupenda, hubirini pande zote Bwana anatupenda, lisifuni Jina lake Bwana anatupenda

  3. Bwana ametuokoa Ametubariki, ametupa vitu vyote Ametubariki, ametulinda salama Ametubariki

  4. Nguvu enzi na uwezo Ni wake milele, nguvu-u na utawala Ni wake milele, madaraka na ufalme Ni wake milele

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page