top of page

Nitaimba na Kumtukuza Muumba Wangu


Nitaimba na kumtukuza muumba wangu hata nizeeke, nitembee na fimbo, nitembee na fimbo ili nimsifu Bwana Mungu wangu x2

Mama Maria nakubembeleza, Mama Maria unisaidie, uniombee (Mama) kwa Mwanao Yesu, niishi siku nyingi (ili) nimsifu Bwana x2

  1. Nitalitangaza neno la Bwana bila aibu, milele na milele mpaka nitembee na fimbo.

  2. Nitalihubiri neno pande zote ulimwenguni, milele na milele mpaka nitembee na fimbo.

  3. Atukuzwe Baba na Mwana nae Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele.

73 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page