top of page

Nitaijongea Meza Yako

Nitajongea meza (yako) Bwana nikupokee (Mungu wangu) umenialika mimi (kwenye) karamu yako. Mwili pia damu yako (Yesu) ndio uhai wangu (siku zote) kaa ndani mwangu Bwana (nami) ndani mwako.

  1. Ninakutamani Yesu, uingie moyoni mwangu, kama vile ayala, atamanivyo maji ya kijito.

  2. Nafsi yangu hudhohofika, nisipokula mwili wako, najihisi nanyauka, nisipokunywa damu yako.

  3. Nina simama imara, ninapokula mwili wako, ninasimama imara, ninapokunywa damu yako

  4. Naye shetani muovu, hutorokea mbali nami, nao ma-adui zangu, husonga songa mbali nami.

  5. Yesu unapoingia na kukaa ndani mwangu mimi, kamwe siogopi kitu kwani wewe ndiwe kinga yangu.

0 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page