top of page

Nipishe Njia


  1. Nipishe njia nipeni nafasi- Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi nitamwimbia ngoma nitacheza- Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi Natamani kuruka, nifika kule, Nimuinue Mungu kwa mikono yangu, Nimueleze kwa kinywa, changu mwenyewe, Kwamba nimefurahi kwa upendo wake, Bwana nashukuru, nashukuru nashukuru tu Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho, Sina cha kusema, cha kusema cha kusema tu, Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho

  2. Kaniinua kutoka shimoni -Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi akaniweka juu ya kinara - Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

  3. Nitazunguka kwa maringo tele - Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi na tabasamu lisilo kauka - Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

  4. Nitawashika wenzangu mikono - Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi tujiinue juu kwa pamoja -Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

  5. Wenzangu si mmejionea wenyewe - Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi, Mungu alivyo mwema wa ajabu -Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

  6. Nitaandika utukufu wake - Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi na wajukuu wangu wausome -Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

16 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page