top of page

Ninakupenda Ewe Mwokozi

Ninakupenda ewe Mwokozi wangu,

rafiki yangu mpenzi wa moyo wangu,

Ukae nami daima ndani yangu,

nipate nguvu na heri siku zote.


Nina kutolea mwili na roho yangu, unipe neema zako nipate nguvu, Nikae nikupendeze mwokozi wangu, shetani muovu kamwe asinipate.


Nilinde niwe imara na mwenye nguvu, nisitumbukie tena katika dhambi, Unionyeshe yaliyo ya heri kweli, nipate kuishi kwa kumpendeza Bwana


Nawe uliye njia kweli na uzima, niongoze vyema daima siku zote,

Uniangazie mwanga palipo giza, nifikishe kwake Baba kwa neema yako


Nakukaribisha Bwana moyoni mwangu, nijarie ewe Bwana baraka yako, Hata siku ya mwisho nitakuapia, ni ile mbinguni kwenye heri milele.

16 views0 comments

コメント

5つ星のうち0と評価されています。
まだ評価がありません

評価を追加
bottom of page