top of page

Ninakuabudu Mungu Wangu


  1. Ninakuabudu Mungu wangu Unayejificha altareni Ninakutolea moyo wangu Usiofahamu siri yako

  2. Mafahamu yangu yadanganya Yanapokuona na kugusa Namsadiki Yesu hadanganyi Yeye Mungu Mwana na Ukweli

  3. Waficha umungu msalabani Na ubinadamu altareni Nami naungama yote mbili Kama mwivi yule mwenye toba

  4. Tomaso aligusa majeraha Nami nasadiki bila shaka Ewe Yesu nipe pendo lako Tumaini kwako na imani

  5. Umeteswa nini Bwana mwema Kwaku nipa mkate wauzima Yesu unifiche ndani yako Ili nilionje pendo lako

  6. Yesu pelikane nitazame Na kwa damu yako nitakase Tone moja ndilo linatosha Na dunia yote yaokoka

  7. Ndani ya mafumbo Yesu yumo Atafumbuliwa kwangu lini NikuoneYesu usowako Nishiriki nawe heri yako AMINA.

31 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page