top of page

Nimemuona Yule

Nimemuona yule ninayemtafuta na neema, zake (nimemuona) leo nimemuona Mungu x 2

(Mikononi mwake) Anauzima tena ni wa milele, Mkononi mwake anauzima ninao utafuta,

Na uzima huo anatoa bure kwa walio tayari, lakini kuna kanuni moja ya kwamba huwajali watu.


Nimemuona Mungu ni mtupu hana nguo, anatamani mimi niende nikamvishe,

nimemuona Mungu ana njaa hana chakula, anatamani mimi niende nikamlishe,

nimemuona Mungu anaumwa kitandani, anatamani mimi niende kumtazama.


Nimemuona Mungu amefungwa gerezani, anatamani mimi niende kumfariji,

nimemuona Mungu nimkimbizi mpakani, anatamani mimi niende kumpokea,

nimemuona Mungu niyatima hana wazazi, anatamani mimi niende nikamtunze


Nimemuona Mungu ni mjane hana mchumba, anatamani mimi niende nikamhifadhi,

mimemuona Mungu amefiwa ana majonzi, anatamani mimi niende kumfariji,

nimemuona Mungu ni kulema hajiwezi, anatamani mimi niende kumuinua


Nimemuona Mungu anatolewa angali mimba, anatamani mimi niende kumtetea,

nimemuona Mungu anapigwa kwa makombora, anatamani mimi niende kusuluhisha.

1 view0 comments

Коментарі

Оцінка: 0 з 5 зірок.
Ще немає оцінок

Додайте оцінку
bottom of page