top of page

Nimelemewa na Hatia Zangu

1. Nimelemewa na hatia zangu, nakutamani kufika mbinguni,

Ingawa mwenye dhambi haingii, iko sauti yaniita nije.

(Naja) Naja kwako Yesu Bwana, (Nisa) Nisafishe dhambi zangu.

2. Mimi mchafu nitaweza wapi, kufika kwenye nchi takatifu,

Kitini mwa enzi nisimame, iko sauti yaniita nije.

3. Ingawa natamani kuifuata, njia ya haki dhambi yanipiga,

Lakini nasikia neno njema, tubu na wewe utusamehewa.

4. Sauti yako Yesu nasikia, mikono yako yanivuta leo,

Na damu yako yasafisha dhambi, na kuniweka mbele yako Bwana.

32 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page