top of page

Nimeahidi Yesu


1. Nimeahidi Yesu, kukutumikia, wewe u Bwana wangu, u rafiki pia, sitaogopa vita, wewe ndiwe mweza, sitaiacha njia, ukiniongoza

Imbeni aleluya, aleluya imbeni, shangwe kwa Bwana Yesu, ndiye mweza wetu

2. Dunia i karibu, Bwana siniache, na mengi majaribu, yako pande zote, siku zote adui, ni ndani na nje, Bwana Yesu nivute karibu na wewe.

3. Nikusikie wewe, nena nami Bwana, kelele za dunia ndizo nyingi sana, nena kunihimiza au kunionya, nena nikusikie, mwenye kuniponya.

4. Umewapa ahadi wakufuatao, kwenda uliko wewe, wawe huko nao, nami nimeahidi, kukutumikia, nipe neema Bwana ya kukwandamia.

5. Hatua zako Bwana, na nizikanyage, wewe u mwenye nguvu, mimi ni mnyonge, niongoze nivute, nishike daima, mwishoni niwasili mbinguni salama.

4 views0 comments

コメント

5つ星のうち0と評価されています。
まだ評価がありません

評価を追加
bottom of page