top of page

Nilaki Mama Maria

1. Maria Mama wa Yesu siku zimepita, natamani kuwa nawe huko juu mbinguni, (Nakuishi pamoja na watakatifu) x2


Nilaki (Maria) nilaki (ee Mama), nilaki mlangoni mwa mbingu x2


2. Yesu Mwana wa Maria alinifia mimi, alimwaga damu yake, kuniokoa mimi, (shetani naye anataka nipotee) x2.


3. Mimi mwenye dhambi mimi, nakulilia wewe, niombee kwa Mwanao, ili nihurumiwe, (nakimbilia uwezo wako ee Mama) x2


4. Nikifika huko juu nitakubusu Mama, nitaimba aleluya Mwokozi asifiwe, (nitaimba pamoja na watakatifu) x2


5. Mungu Baba Mungu Mwana na Roho Mtakatifu, ndiye mkuu wa majeshi huko juu mbinguni (nitakuimbia na kukusifu milele.) x2.

10 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page