top of page

Nikushukuruje Bwana



Ee Mungu wangu nakushukuru umenitendea mema mengi Bwana Asante, asante, Mungu wangu nashukuru x2


Mungu wangu ninakushukuru kwa upendo na wema wako Bwana, sijui mimi nikushukuruje Bwana kwa fadhili ya wingi wa fadhili zako x2 ukarimu wako


1. Bwana Mungu wangu Mungu wa Abraham uliyegawanyisha bahari ya shamu, wana wa Israeli wakavuka salama umedhihirisha wema wako kwangu (Bwana)


2. Unaninyeshea mvua ya Baraka nakuniangazia nuru ya uso wako, umenizungushia nyimbo za ushindi wema wako kwangu hauna kipimo (Bwana)


3. Umenijalia familia bora ilojaa upendo na moyo wa Imani, umenizawadia na marafiki wema na wanishikao mkono kwa upendo (Bwana)


4. Siku zote Bwana unanilinda vyema chini ya mbawa zako Bwana niko salama, nikukoseapo Bwana wanisamehe na kunirejesha kwako kwa upole (Bwana)


5. Leo ninaimba wimbo wa shukrani, kwa kinywa changu Bwana ninasema asante, milele na milele nitakusifu wewe na kusimulia ukarimu wako (Bwana)

94 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page