top of page

NIkupe Nini Mungu Wangu



Nikupe nini Mungu wangu, nikupe nini we Mwokozi Nikupe nini Bwana wangu cha kukupendeza ) x2

  1. Kila nitakachoshika mbona bado ni kidogo Fadhili unazotenda kwangu mimi naogopa Ninakuomba Mwokozi, nifanyie msamaha na unipokee Mema unayoyatenda, nitafanya nini mimi nikurudishie

  2. Nakutolea mkate toka mmea wa ngano Nakutolea divai ni tunda la mzabibu Ninakuomba Mwokozi . . .

  3. Mchana hata siku wewe wanisimamia Na nikiwa safarini waniepusha ajali Ninakuomba Mwokozi . . .

  4. Nikiwa na matatizo Bwana wanisaidia Nikiwa kwenye majonzi Bwana unanifariji Ninakuomba Mwokozi . . .

  5. Kama njia siioni Bwana unaniongoza Na hata nikipotea kwako unanirudisha Nitatoa nini mimi, kitakachokuwa sawa, na fadhili zako Nitaimba vipi mimi, niyataje mema yote, utendayo kwangu

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page