top of page

Nikupe Nini Ee Mungu


Nikupe nini ee Mungu cha kukupendeza Uwezo wangu mdogo Bwana waujua pamoja na dhiki inayonisonga Pokea zawadi yangu hii duni

  1. Nikitazama wenzangu wanakutolea Zawadi nyingi na nzuri za kukupendeza kasoro mimi tu natoa kidogo Wakati mwingine sitoi kabisa

  2. Maisha yangu ya dhiki Bwana wayajua Unyonge na udhaifu wangu waujua Sina kitu mimi cha kukutolea Lakini pokea nafsi yangu Bwana

  3. Nayakabidhi maisha yangu kwako Bwana Uniongoze katika njia za uzima unisaidie wakati wa shida Kwani ni wewe tu tumaini langu

  4. Kutoa ndugu ni moyo sio utajiri Ukimtolea Mungu atakuongeza uwasaidie watu maskini Wasiojiweza utabarikiwa

  5. Ninawasihi wenzangu mliojaliwa Maisha bora mazuri na ya kuridhisha msimsahau Bwana Mungu wenu Toeni kwa wingi mtabarikiwa.

2 views0 comments

コメント

5つ星のうち0と評価されています。
まだ評価がありません

評価を追加
bottom of page