top of page

Nikupe Nini Bwana

Nikupe nini Bwana cha kukupendeza,(ama)nikutolee nini chakufurahisha Ni mema mengi Bwana umenitendea (mimi) sina budi kusema asante kwa yote.(Nina kuja kwako Bwana ninaleta zawadi japo ni kidogo sana Bwana upokee x2)

1.Mazao ya mashamba Bwana tunakutolea ni matunda ya jasho letu upokee.

2.Mkate na divai Bwana tunakutolea,ukageuze mwili na damu ya yesu.

3.Na fedha za mifuko Bwana tunakutolea,ni kazi ya mikono yetu upokee.

4.Hata na nafsi zetu Bwana tunakutolea,ni sura na mfano wako Bwana Mungu.

6 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page