top of page

Nikupe Nini

1. Nikupe nini ee Mungu cha kukupendeza uwezo wangu mdogo Bwana waujua.

Pamoja na dhiki zinazonisonga, pokea zawadi yangu hii duni.

2. Nikitazama wenzangu wanakutolea, zawadi nyingi na nzuri za kukupendeza,

Kasoro mimi tu, natoa kidogo , wakati mwingine sitoi kabisa.

3. Maisha yangu ya dhiki Bwana wayajua, unyonge na udhaifu wangu waujua.

Sina kitu mimi cha kukutolea, lakini pokea nafsi yangu Bwana.

4. Nayakabidhi maisha yangu kwako Bwana, uniongoze katika njia ya uzima.

Unisaidie wakati wa shida, kwani ni wewe tuu, tumaini langu.

5. Kutoa ndugu ni moyo sio utajiri, ukimtolea Mungu atakuongeza.

Uwasaidie watu masikini, wasiojiweza utabarikiwa.

6. Nina wasihi wenzangu mliojaliwa, maisha bora mazuri naya kupendeza.

Msimsahau Bwana Mungu wenu, toeni kwa wingi mtabarikiwa.

0 views0 comments

Comentários

Avaliado com 0 de 5 estrelas.
Ainda sem avaliações

Adicione uma avaliação
bottom of page