top of page

Nifanyeje Mimi

Nifanyeje mimi Ee Mungu wangu nijonge meza yako, nifanyeje mimi Ee Mungu wangu nishiriki karamu yako Kwani moyo wangu Bwana unatamani kula chakula..lakini sistahili kuijongea meza yako. (Nifanyeje mimi ee Bwana nile chakula chako) x2

1. Mwili wako ee Bwana Yesu ni chakula cha uzima, kilichoshuka kutoka mbinguni ni chakula cha uzima.

2. Damu yako ee Bwana Yesu ni kinywaji cha uzima, niutakaso wa Roho zetu, damu yako ndiyo dawa.

3. Bahati gani tumepewa na Bwana wetu Yesu, kula mwili na kunywa damu yake nijongee kwa furaha.

4. Umenialika kujongea kwenye karamu yako, karamu yako, karamu yako ya upendo nijalie nipatie.

0 views0 comments

Commentaires

Noté 0 étoile sur 5.
Pas encore de note

Ajouter une note
bottom of page