top of page

Ni Salama Rohoni Mwangu

Nionapo amani kama shwari Au nionapo shida; Kwa hali zote umenijulisha Ni salama rohoni mwangu (Salama) salama rohoni, ni salama rohoni mwangu x2 Ingawa shetani atanitesa Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu Amekufa kwa roho yangu (Salama) salama rohoni, ni salama rohoni mwangu

Dhambi zangu zote, wala si nusu Zimewekwa Msalabani Wala sichukui laana yake Ni salama rohoni mwangu (Salama) salama rohoni, ni salama rohoni mwangu Ee Bwana himiza siku ya kuja Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Nisalama rohoni mwangu (Salama) salama rohoni, ni salama rohoni mwangu

15 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page