top of page


Ni mazao ya mashamba nazo fedha za mifuko ni mkate na divai tunaleta kwako Baba x2

  1. Leo tuko hima na tumejawa furaha (sisi) tunaimbaimba na tunachezacheza. Tumekata kauli tunaenda kwa Bwana (leo) twarudisha talanta tuliyojaliwa.

  2. Wiki nzima Mungu ametulinda salama (kweli) akatuhepusha nazo hatari zote. Mashamba yetu yote ameyarutubisha (kweli) mvua inanyesha na jua linawaka.

  3. Ngombe wetu kondoo na mbuzi wanazaa (kweli) hata kuku na bata wataga mayai. Ametujalia nguvu za kufanya kazi (kweli) sisi tunakula na tena tunashiba

  4. Mkate wa ngano divai ya mzabibu (Bwana) ugeuze mwili na damu yake Yesu Tutakula mwili pia tutakunywa damu (kweli) sisi tutapata uzima wa milele

  5. Nitakupa nini Bwana cha kukupendeza (kwani) uliyonitendea hayana kipimo. Pokea zawadi yangu japo ni kidogo (Bwana) wewe wanijua mpaka moyoni mwangu.

7 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page