top of page

Ni Maria Mtakatifu

Ni Maria Mtakatifu - Tumshangilie Maria

Ni mzazi wa Mungu mwana - Tumshangilie Maria

Ni mkuu wa mabikira - Tumshangilie Maria

Ni Mama yake Yesu Kristu- Tumshangilie Maria


Vigelegele vifijo na makofi……Hoi hoi nderemo (nyingi) pia vifijo tumshangilie, Mama Maria. Yeye ni mwombezi (wetu) na msaada budi tumwimbie, chereko mama


Mama wa neema ya Mungu- Tumshangilie Maria

Mama Mtakatifu sana- Tumshangilie Maria

Mama wa usafi wa moyo - Tumshangilie Maria

Ni Mama asiye na doa - Tumshangilie Maria

Ni Mama asiye na dhambi - Tumshangilie Maria

Ndiye Mama mpendelevu - Tumshangilie Maria

Ni Mama mstaajabivu- Tumshangilie Maria

Ni Mama wa shauri jema - Tumshangilie Maria


Ndiye Mama wake muumba - Tumshangilie Maria

Ndiye Mama wa Mkombozi- Tumshangilie Maria

Bikira wa utaratibu- Tumshangilie Maria

Ni Bikira mwenye heshima - Tumshangilie Maria

Ndiye Bikira mwenye sifa- Tumshangilie Maria

Ndiye Bikira mwenye enzi - Tumshangilie Maria

Ni Bikira mwenye huruma - Tumshangilie Maria

Na ndiye Bikira amini - Tumshangilie Maria

Na ndiye kioo cha haki - Tumshangilie Maria

Ni kikao chenye hekima- Tumshangilie Maria

Sababu ya furaha yetu- Tumshangilie Maria

Ndiye chombo chenye neema - Tumshangilie Maria

Ndiye chombo chenye heshima - Tumshangilie Maria

Ni chombo bora cha ibada- Tumshangilie Maria

Ndiye waridi lenye fumbo - Tumshangilie Maria

Ndiye mnara wa Daudi- Tumshangilie Maria

16 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page