top of page

Ni Harusi Leo

1a. Nasikia kelele na vigelegele nauliza kweli kuna nini (leo)

b. Nawaona walio na mavazi mazuri wanavyotembea kwa maringo (leo)


Ni harusi pigeni kelele, ni harusi pigeni makofi, ni harusi tuimbe kwa shangwe na vigelegele tupige


2a. Tazameni bwana anavyopendeza, anavyokanyanga polepole- (sana)

b. Naye bibi harusi anametameta, amepambwa maua- (sana)


3a. Nyanyueni bendera mikononi mwenu, mzipeperushe kwa pamoja- (wote)

b. Simameni tucheze kwa furaha wanapoingia, tuimbe kwa shangwe – (wote)


4a. Ewe bwana harusi mpende mke wako, siku zote umlinde – (vyema)

b. Nawe bibi harusi mheshimu mume wako , siku zote umtunze- (vyema)

12 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page