top of page

Nguvu ya Mazungumzo


  1. Mimi si mkamilifu ni mwanadamu, nawe si mkamilifu ni mwanadamu. Mbona tunakoseana twaumizana lakini tusikubali kuchukiana (njoo)

  2. Amani ni jambo jema na muhimu, (jambo muhimu), inaimarishwa kwa mazungumzo (mazungumzo) ikitetereka ihangaikiwe. Na Imani ni tunda la haki, tuzungumze tutendeane haki, karibu njoo (njoo)

  3. Niwe na moyo mwepesi kuomba radhi, niwe mwenye kuelewa na kusamehe, niwe msahaulifu nikikosewa, na mwenye kukumbuka ninapokosea (njoo)

  4. Mbinguni watafurahi wakiona, tuliokwaruzana tunaongea, na tunamaliza tofauti zetu. (njoo)

3 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page