top of page

Ngoja Nicheze


Tazama mimi ninavyopumua, Tazama mimi nilivyo na nguvu Tazama mimi ninavyopumua, Tazama mimi nilivyo na nguvu Hizo zote - ni neema bure toka kwa Mungu Na mimi leo - ngoja nicheze muone, Nitamsifu ngoja nicheze muone, bila kuchoka - ngoja nicheze muone aee

  1. Tazama mimi nakula na kushiba, Tazama mimi nalala nasinzia Tazama naamka mimi mwenyewe, Tazama tazama ah tazama aa aha

  2. Tazama mimi naweza kuongea, Tazama mimi naimba bila shida Tazama naweza kucheza mwenyewe, Tazama tazama ah tazama aa aha

  3. Nikiugua ona napewa pole, ninapofiwa ndugu mwanifariji Tazama niwapo na shida wanajaa tazama tazama ah tazama aa aha

  4. Nikikosea huwa nasamehewa, nikiudhiwa ndugu mwanitetea Tazama dhuluma haitaniua tazama tazama ah tazama aa aha

  5. Nikifurahi ndugu washerehekea, nikiudhiwa ndugu wasononeka Tazama ninaishi kati ya watu tazama tazama ah tazama aa aha

  6. Na yote haya najaliwa na Mungu, Amenipenda upeo wa upendo Tazama na mimi nitamtukuza, Tazama tazama ah tazama aa aha

1 view0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page