top of page

Neema Zimetiririka



Zimetiririka zimetiririka, Zimetiririka neema za Mungu


Zimetiririka, neema zimetiririka, neema zimetiririka wote tumeinuliwa aleluya x2

{Majumbani mwetu (zimetiririka) Mashambani mwetu (zimetiririka tiririka) Familia zetu (zimetiririka) tumeinuliwa aleluya} x2


Tazama mimea inavyochanua, hizi ni neema kutoka Mbinguni


Tazama bahari na mawimbi yake, vinashangilia neema za Mungu


Tazama wanyama wanavyopendeza, ndege wa angani wanaburudisha


Mvua inanyesha jua inawaka, kuukamilisha utukufu wake


Mchana na usiku vinatuongoza, kuyafurahia majira ya mwaka


Mbingu zafurahi na mawingu yote, vinashangilia neema za Mungu

11 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page