top of page

Nasonga Mbele




(Baraka zake (Mungu tu) zinanitosha faraja zake zanipa nguvu, neema zanibariki mkono wake waniongoza (Kwa ujasiri) Nasonga mbele polepole kwa Imani na utumishi sirudi nyuma tena asilani Nasonga mbele polepole kwa Imani (hehe) sirudi nyuma tena asilani (Songa mbele) nasonga mbele polepole kwa Imani hehe sirudi nyuma tena asilani nasonga mbele


  1. Tazama Mungu ni mwema tazama ni mwenye neema Bwana rehema zake ni adili Mungu wangu nitamsifu daima, Tazama ananilinda tazama ananipenda sana na nafsi inaburudika kazi yangu nikumsifu daima (Mungu wa haki yangu)

  2. Tazama ndege angani daima wanamsifu Bwana kwa nini nisimuimbie Mungu wangu nitamsifu daima. Tazama hata wanyama mwituni wanafurahi sana kwa nini nisifurahie kazi yangu nikumsifu (Mungu wa haki yangu)


HITIMISHO

Ee nafsi uzidi kumsifu Bwana Ee nafsi yangu msifu Bwana kwa shangwe usisahau fadhili na heri kwetu sisi mrudishie Bwana kwa moyo mweupe naye Bwana Mungu atakubariki naye Bwana Mungu atakubariki aeeh, sitarudi nyuma mimi kukushukuru mimi nasonga mbele kukuimbia sitarudi nyuma mimi kukutukuza mimi nasonga mbele kukuinua Bwana

10 views0 comments

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
bottom of page